BWANA WA MAJESHI by GLORIOUS WORSHIP TEAM (GWT) LYRICS

BWANA WA MAJESHI by GWT LYRICS
Bwana wa majeshi leo uinuliwe
Wee baba uinuliwe ee
Wee Mungu uinuliwe ee uinuliwe ee

VERSE 1
Uliumba mbingu na nchi uinuliwe
Mfalme wa wafalme Mungu mwenye nguvu
Baba wa milele Baba uinuliwe
Nani aliye kama wewe Baba wa milele
Mungu mwenye huruma mwenye upendo Mungu wangu
Nalisifu jina lako pekee yako
Hakuna aliye kama wewe baba yangu baba


CHORUS
Bwana wa majeshi leo uinuliwe
Wee baba uinuliwe ee
Wee Mungu uinuliwe ee uinuliwe ee


VERSE 2
Wewe ni Mungu uliyeniponya na kaburi
Wewe ni Mungu mponyaji
Nalisifu jina lako Nakuabudu baba Leo uinuliwe
Nani aliye kama wewe Baba wa mbinguni
Mungu mwenye huruma mwenye upendo Mungu wangu
Nalisifu jina lako pekee yako
Hakuna aliye kama wewe baba yangu baba