NIMERUDI TENA LYRICS -PRAISE TEAM TAG FOREST YA KWANZA

Bwana nimerudi tena
Yesu nakushukuru
Wengine sijui ila mimi Bwana
Nimejua umenitendea

Nimeomba mengi umenijibu moja
umetutendea wengi mimi nimerudi
Japo mengine bado
Ila natambua thamani ya hili moja ulilotenda

Wale wengine kenda mimi sijui
Ila nachojua kwangu umetenda
Wengine sijui ila hili Bwana
nimejua umenitendea

Mimi ni msamaria tu 
Mtu wa makabila mengine
Wala sikustahili haya uliyonitendea
Wengine sijui wanaona nini
Ila mimi Bwana 
Ninauona wema wa ajabu

Wenye ukoma tulikua kumi
Na neno lako halikufanya makosa
Wengine sijui ila mimi bwana 
Ninajua umenitendea

Wenye dhambi tulikua wengi
Na damu yako ikanitakasa
Wengine sijui ila mimi bwana 
Ninajua umenitendea

Utukufu (Kwako tu)
Na heshima zote (Kwako tu)
Umenitenda wema
Umenitenda vyema
Umenitendea wema tu

Umenitenda wema
Umenitenda vyema
Umenitendea wema tu