Malaika Lyrics By Msanii Music Group

Kisa cha Mafarisayo chashangaza 
Walimshika Yesu, wakamsulubisha
Wakamlaza kaburini, kisha wakaweka jiwe kubwa 
Wakajua yamekwisha 
Ndivyo watu wengi, maadu zetu
Wanayaweka mawe, wakidhani wamezifunga njia
Wanaiweka mitego, ili tuanguke
Wasilo lijua: tumezungukwa na malaika
Wasilo lijua: tumezungukwa na malaika, wa nuru

Ni malaika aliondoa jiwe kaburini
Mwana wa Mungu asiye na hatia kainuliwa
Jaribu linaweza kuwa kubwa kwetu
Ila Mungu huleta mlango wa kutokea
Jaribu linaweza kuwa kubwa kwetu
Ila Mungu huleta mlango wa kutokea

Walimuua Yesu, kisha wakaweka jiwe
Kubwa, asiweze kufufuka
Asikari nao walikesha kule
Mwili wake usipate kuibiwa 
Maadui hata wakeshe, neno la Mungu linatimia
Mipango yake hukamilika, ahadi zake hazichelewi 
Ni mwaminifu Mungu wetu, ni mwaminifu
Ni mwenye Nguvu Mungu wetu, yeye hashindwi