Neno Litasimama Lyrics by Msanii Music Group

Neno litasimama
Neno litasimama
Mambo yote yatapita 
Lakini neno litasimama

Vitabu vingi sana vimeandikwa
Kwa hekima yake mwanadamu 
Vikitupotosha waziwazi 
Vile twaweza kuishi vyema duniani
Ila yabidi tuelewe 
Kwamba pale mwanzo kulikuwa Neno 
Na Neno alikuwapo kwa Mungu 
Naye Neno alikuwa Mungu 



Warembo wote watapita
Wanaume mali safi watapita 
Wamamas wababas watapita
Lakini neno lake Mungu litasimama 
Bale mpya zitapita 
Wale wameweza watapita
Raha za dunia zitapita 
Lakini neno litasimama 



Ugumu wa dunia utapita 
Mali ya dunia yatapita 
Na utajiri wote utapita 
Lakini neno lake Mungu litasimama 
Vyeo vya kisifa vitapita 
Na falme zote zitapita 
Vilivyodhaminiwa na vitapita 
Lakini neno lake Mungu litasimama