Nikaiona huko
Neema kubwa kama mto,
Neema ya ajabu.
Neema ya Golgotha
Ni kama bahari kubwa,
Neema tele na ya milele,
Neema ya kutosha!
Nilipofika moyo wangu
Ulilemewa sana,
Sikufaamu bado vema
Neema yake kubwa.
Nilipoona kwamba Yesu
Alichukua dhambi,
Neema ikadhihirika,
Na moyo ukapona.
Mbinguni nitakapofika,
Furaha itakuwa
Kuimba juu ya neema
Milele na milele.
Social Plugin