DAMU YAKO YENYE BARAKA - PAPI CLEVER & DORCAS Ft MERCI PIANIST



Damu yako yenye baraka inayo tuosha makosa,
Ilitoka msalabani, Bwana Yesu, ulipokufa. 
Nastahili ‘pata hukumu, na siwezi mimi kujiosha. 
Unioshe katika damu nipate kuwa safi kabisa


Safi, safi kweli, safi, safi kweli! 
Unioshe katika damu, 
nipate kuwa safi kabisa!


Yesu, ulivikwa miiba, kuangikwa juu ya mti. 
Ulivumilia mateso, maumivu na majeraha. 
Ninataka kijito hicho, n’ende na nikasafishwe sana! 
Unioshe katika damu, nipate kuwa safi kabisa.


Baba, kweli nina makosa, moyo wangu wa udhaiffu;
Mimi mwenye dhambi rohoni nitaona wapi Mwokozi? 
Yesu, kwako msalabani naja, ninakuamini sasa. 
Unioshe katika damu,, nipate kuwa safi kabisa.


Bwana,, nimefika karibu,, unilinde kwako milele! 
Ufungue kila kikamba, unijaze moyo mwenyewe. 
Na karibu ya msalaba nitakaa hata kufa kwangu. 
Unioshe katika damu,, nipate kuwa safi kabisa