ROHO YANGU INAIMBA LYRICS BY PAPI CLEVER & DORCAS ft. MERCI PIANIST

Nimefika kwake Yesu
Na rohoni mwangu sasa
Jua lake la neema 
Linang’aa kila siku

Chorus 
Roho yangu inaimba
Nimefunguliwa kweli
Nimekaribia Yesu
Ninaimba kwa furaha. 

Pepo za neema yake 
Zinavuma ndani yangu
Na mawimbi ya wokovu 
Yananijaliza sasa

Sasa Bwana Yesu Kristo 
Amefanya kao kwangu
Nimepewa mfariji
Roho ya ahadi yake

Siku roho afikapo 
Mtajua kwa hakika 
Kwamba ninakaa kwenu
Hivyo Yesu alisema

Kweli, amefika kwetu, sasa yumo ndani yetu. 
Ujitoe kwake Mungu, aioshe roho yako

Yesu atakapokuja katita utakatifu, nitafananishwa naye,
Nitamshukuru sana. 

Chorus 2 
Zitakuwa nyimbo nyingi tuta’poingia mbingu, 
Na milele tutaimba na kusifu Mungu wetu.