Usisahau Lyrics By Ufunuo Choir

Chorus
Usisahau hata kidogo
Usisahau kumshukuru 
Yale yote Mungu aliyo kutendea 
Usisahau kumshukuru Mungu

 Verse 
Basi hapo moyo wako wewe 
Usiinuke ukamsahau Mungu wako 
Aliye kutoa katika nchi ya Misri 
Aliye kutoa katika nyumba ya utumwa

Aliye kuongoza katika jangwa lile kubwa 
Lenye vitisho, lenye nyoka za moto 
Lenye nge, nchi yenye kiu 
Nchi ‘siyokuwa na maji

Aliye kutolea maji kata mwamba mgumu sana 
Aliye kuongoza njia katika safari yako 
Aliye kulisha jangwani kwa mana, mana 
Wasio ijua baba zako

Refrain
Katika mema yako 
Na katika mafanikio yako 
Wala usiseme moyoni mwako “Nguvu zangu 
Na uwezo wangu, ndio uliyonipatia 
Utajiri huu

Refrain 2: 
Bali mkumbuke Bwana wako maana 
Ndiye akupae nguvu za kupata utajiri 
Ili afanye imara 
Agano lake Bwana, Mungu

Basi yatupasa kutambua 
Bwana Mungu ndiye, ndiye 
Atanguliaye mbele yako kama moto 
Uteketezao, na kuangamiza 
Walio watesi wako (wako, wako, wako)

Bali mkumbuke Bwana wako maana 
Ndiye akupae nguvu za kupata utajiri 
Ili afanye imara 
Agano lake Bwana, Mungu

Usisahau hata kidogo 
Usisahau kumshukuru 
Yale yote Mungu aliyo kutendea 
Usisahau kumshukuru Mungu